UIMARA wa kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra nyuma yupo mtaalamu wa mbinu anaitwa Milton Nienov.
Sio mdaka mishale tu hata Metacha Mnata pia ambaye ni kipa namba mbili kwa sasa ananolewa na kocha huyu.
Erick Johora na Aboutwalib Mshery ambaye bado hajwa imara akirejea atakuwa mikononi mwa kocha huyu.
Katika upande wa ulinzi eneo hili Yanga wameipiga hatua kubwa kitaifa na kimataifa.
Kwenye Kombe la Shirikisho Afrika mabao manne pekee wametunguliwa katika hatua ya makundi na mchezo wa kwanza wa robo fainali hawajatunguliwa zaidi ya kupata ushindi.
Kwenye Ligi Kuu Bara Yanga ni timu namba moja kuruhusu mabao machache ambayo ni 13 baada ya kucheza mechi 26.
Kituo kinachofuata Jumapili, Yanga v Rivers United mchezo wa robo fainali ya pili utakaotoa maamuzi ya timu itakayotinga hatua ya nusu fainali itakuwa ni Aprili 30,2023.
Yanga wametanguliza mguu mmoja baada ya ushindi kwenye mchezo uliopita ubao uliposoma Rivers United o-2 Yanga.