BONDIA Twaha Kiduku amechapa Lago Kiziria kutoka Georgia kwa pointi na kufanikiwa kutetea taji lake la UBO huku akishinda taji jipya la PST hapa katika Ukumbi wa Tanzanite, Morogoro.
Baada ya ushindi huo Twaha ambaye ni mzawa ameweka wazi kuwa furaha ya ushindi ni kubwa na hatarudi nyuma kwa kuwa anahitaji kufanya vizuri zaidi.
“Wamezoea huwa sirudi nyuma, leo nimewachanganyia kidogo na ni furaha kwetu kupata ushindi na hii ni zawadi kwa mashabiki wangu wote na kazi bado inaendelea.
“Ilikuwa ni pambano kubwa na gumu ila mwisho kazi imeonekana kwani haikuwa kazi rahisi kufanikiwa katika hili,”.
Ilikuwa ni Usiku wa Vitasa Mfalme kwenye Ufalme wake.