SALIM PONGEZI SAWA LAKINI TIMU INAZIDI KUIMARIKA

ANGALAU kwenye ukuta wa Simba kuna makosa yanazidi kufanyia kazi hasa eneo la ulinzi ambalo limekuwa lifanya makosa mengi makubwa yanayoigharimu timu.

Ukimpongeza Ally Salim kwenye mechi tatu ambazo amekaa langoni ukamuweka kando nahodha Mohamed Hussein bado utakuwa hujatenda haki.

Ipo wazi kwamba kwenye mchezo dhidi ya Yanga, Mohamed alifanya makosa mengi ambayo yalimpa mtihani mzito Salim ila kwa bahati mbaya mfungaji Fiston Mayele alikosa bahati ya kumtungua.

Joash Onyango akiwa ndani ya 18 ni mwepesi kucheza faulo jambo amalo lilimpa kadi ya njano kwenye mchezo dhidi ya Wydad Casablaca lakini naye amezidi kuimarika.

Pongezi kwa Shomari Kapombe, makosa anafanya kisha anasahihisha haraka nje ya 18, ushindi dhidi ya Wydad ni ishara tosha kwamba makosa yanaoreshwa na kuwa fursa.

Kete ya kwanza imegota mwisho na ile ya pili ugenini ni ngumu kuliko ile ya Uwanja wa Mkapa, kila la kheri Simba wawakilishi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Bado kwenye eneo la kipa ndani ya Simba ni muhimu kufanyiwa maboresho maana kipa namba moja Aishi Manula anasumbuliwa na maumivu huku Beno Kakolanya akitajwa kwamba anaweza kuondoka katika kikosi hicho kupata changamoto mpya.

Imeandikwa na Dizo Click.