MATOKEO ya mchezo wa kwanza hayana maana kwamba safari imegota mwisho kwa kila timu bali ni mwendelezo kwenye mchezo unaofuata.
Hakika kwenye mechi za kimataifa wawakilishi wana kazi kubwa kusaka ushindi ili kupata matokeo mazuri ambayo yatawapa furaha mashabiki na Tanzania kiujumla.
Kwa wakati huu kwenye hatua ya robo fainali ni mechi mbilimbili zinachezwa kwa kila timu hivyo ukipoteza mchezo mmoja upo wa mwisho amao huo ni wa kukamilisha matokeo ya jumla.
Simba kete ya kwanza ilikuwa nyumbani dhidi ya Wydad Casablanca kwa walichokivuna bado haijafika mwisho mpaka itakapofika mwisho kwa kuwa wanakwenda ugenini kukamilisha kete ya pili.
Ili kuhakikisha ndoto zinatimia ni lazima kupata ushindi kwenye mchezo wa pili wakiwa ugenini na inawezekana kutokana na mbinu ambazo benchi la ufindi litawapa wacheza.
Kwa wachezaji ni muhimu kuongeza umakini na kutumia nafasi za dhahabu ambazo zinapatikana kwenye mechi ambazo mnacheza uwanjani.
Kwa Yanga wao leo kazi ya kwanza inatarajiwa kuwa dhidi ya Rivers United ni mchezo wa Kombe la Shirikisho wakati Simba wao wapo kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwa kila hatua wawakilishi hawa wamefanya kazi kubwa hivyo ni muhimu kukamilisha safari ya ugenini kwa umakini ili nyumbani kazi iwe moja kutimiza malengo mbele ya mashabiki.
Ugenini ni ngumu kupata ushindi kwa namna ambavyo soa la Afrika lipo lakini ndani ya dakika 90 inawezekana kwa kuwa Yanga walifanya hivyo kwenye mechi ambazo zilipita.
Kila la kheri wawakilishi wetu kimataifa kazi kubwa inahitajika kufanywa na watu wakubwa wakati huu.