SEVILLA HAO NUSU FAINALI

KLABU ya Sevilla imetinga hatua ya nusu fainali Europa League kwa jumla ya ushindi wa mabao 5-2 Manchester United.

Katika mchezo wa robo fainali wa pili wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Manchester United uliochezwa Aprili 20.

Mabao ya Sevilla yalifungwa na Youssef En Nesyri ambaye alipachika mawili dakika ya 8,81 na moja ni mali ya Loic Bade dakika ya 47.

Katika mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Ramon Sanchez Pizjuan United walipiga jumla ya mashuti 16 huku matatu yakilenga lango na wapinzani wao walipiga mashuti 20 huku sita yakilenga lango.