AKILI ZA SIMBA NI KWA WAARABU WYDAD

AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari amesema kuwa kwa sasa ambacho wanakifikiria ni ushindi dhidi ya Wydad  ambao ni hatua ya robo fainali.

Tayari wapinzani hao wamewasili Tanzania Aprili 19 wakiwa kamili kwa ajili ya mchezo huo ambao utachezwa Uwanja wa Mkapa, Jumamosi.

“Hakuna jambo lingine lolote tunaweza kuwaza kwa sasa zaidi ya kumfunga Wydad. Kila Mwanasimba anayo nafasi ya kuisaidia Simba kuandika historia ya kuitoa Wydad.

“Simba ni ya watu, na watu wakiamua jambo lao hakuna linaloshindikana.

“Furaha yetu rasmi itapatikana baada ya kutinga nusu fainali. Hii ya kuwafunga Yanga ni kuwazodoa, malengo yetu ni kwenda nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa. Kuwafunga hawa ambao tumewazidi kila kitu ni kuwakomoa tu, tumeshawafunga sasa tunawaangalia Wydad.

“Mashabiki mkitimiza wajibu wenu kwa kuja uwanjani kushangilia, benchi la ufundi likiwapa maelekezo mazuri wachezaji na wachezaji wakitimiza wajibu wao Wydad hawana pa kutokea.” Ally.