KATIKA orodha ya mastaa wenye pasi nyingi za mabao kiungo wa Simba, Clatous Chama ni namba moja akiwa nazo 14 kibindoni.
Moja kati ya pasi hizo alitoa katika mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya watani wa jadi Yanga, mzunguko wa kwanza Oktoba 23,2022.
Kwenye mchezo huo ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 1-1 Simba na kuwafanya watani hao wa jadi kugawana poiñti mojamoja.
Anayefuata ni Saido Ntibanzokiza yupo ndani ya Simba ametoa pasi 9 za mabao, Ayoub Lyanga wa Azam FC ana pasi 7 za mabao.
Sixstus Sabilo nyota wa Mbeya City yupo na pasi 6 za mabao Nicolas Gyan wa Singida Big Stars ametoa pasi 5 za mabao.
Yanga wao wanaongoza ligi na kinara wa utupiaji mabao yupo pale ambaye ni Fiston Mayele na mabao yake 16 nyota mwenye pasi nyingi ni Aziz KI na Jesus Moloko wanazo pasi nne