KIPA SIMBA AWEKA REKODI YAKE MATATA

ALLY Salim kipa namba tatu wa Simba amekiwasha ndani ya dakika 90 ikiwa ni mchezo wake wa kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara akifanikiwa kusepa na dakika 90 bila kutunguliwa.

Salim hakuwa chaguo la kwanza ndani ya Simba ambapo chaguo la kwanza ni Aishi Manula na namba tatu ni Beno Kakolanya.

Salim hata msimu wa 2021/22 hakupata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza Kati ya mechi 30 ambazo Simba ilicheza.

Wakati ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Ihefu 0-2 Simba, Salim alikaa langoni na kuokoa michomo 10 langoni mwake.

Salim aliokoa hatari dakika ya 5,6,9,10,14,15,16,20,34 na 74 miongoni mwa washambuliaji wa Ihefu ambao walimpa tabu ni Yacouba Sogne ambaye alipiga mashuti manne dakika ya 15,20,71 haya yalilenga lango na dakika ya 65 shuti hili halikulenga lango.

Salim katika mchezo huo alisepa na dakika 90 mazima na kuifanya Simba kuwa timu iliyosepa pointi tatu dhidi ya Ihefukati ya vigogo wawili wa Dar ambao ni Azam na Yanga.

Ikumbukwe kwamba katika ubao huo uliwahi kusoma Ihefu 1-0 Azam FC na Ihefu 2-1 Yanga ilikuwa ngumu kwa vigogo hao kusepa na pointi tatu.