ZAWADI YA PASAKA HII HAPA

MBEYA City wamepoteza dhidi ya Namungo kwa kuacha pointi tatu mazima huku wakiwapa zawadi ya Pasaka mashabiki wao.

Baada ya dakika 90 ubao umesoma Namungo 2-1 Mbeya City.

Mabao ya Namungo yamefungwa na Jacob Masawe dakika ya 23, Shiza Kichuya dakika ya 74 na Mbeya City ni Abdulazak dakika ya 88.

Hiyo ilipigwa Uwanja wa Majaliwa na mchezo mwingine uliochezwa Uwanja wa Jamhuri,Dodoma ilikuwa Dodoma Jiji 1-1 Coastal Union.

Hawa waligawana furaha kwa mashabiki wao ambao walijitokeza kushudia burudani.

Raizin Hafidh alipachika bao dakika ya 87 na Maabad Maulid dakika ya 49.

Tanzania Prisons 3-1 Ruvu Shooting Uwanja wa Sokoine mabao ya Elifadhil dakika ya 6, Jeremia Juma mawili dakika ya 41,50 na lile la Ruvu Shooting lilipachikwa na Valentino dakika ya 02.