JEAN BALEKE AWALIZA IHEFU, ALLY SALIM MIKONO MIA

LICHA ya Ihefu kuwa bora kwenye mchezo wa leo mbele ya Simba kwenye upande wa umiliki wamekwama kusepa na pointi tatu.
Dakika 90 zimekamilika ubao wa Uwanja wa Highland Estate unasoma Ihefu 0-2 Simba.

Mabao yote mawili yamefungwa na Jean Baleke kipindi cha pili katika dakika za lala salama ilikuwa dakika ya 83 na 86.

Mikono ya mzawa Ally Salim ilikuwa kwenye kazi kubwa kuokoa michomo ya Ihefu kupitia kwa Obrey Chirwa na Adam Adam huyu ni nyota wa mchezo kwa leo.

Kipa huyo ni chaguo namba tatu ndani ya Simba katimiza majukumu yake kwa umakini na unakuwa ni mchezo wake wa kwanza ndani ya ligi msimu wa 2022/23.

Simba inafikisha pointi 60 ikiachwa pointi 5 na Yanga iliyo nafasi ya kwanza lakini Yanga ina mchezo mmoja mkononi ikiwa imecheza mechi 24 Simba 25.