YANGA HAO NUSU FAINALI KOMBE LA AZAM SPORTS FEDERATION

YANGA imetinga hatua ya nusu fainali ya Azam Sports Federation kwa ushindi dhidi ya Geita Gold.

Dakika 90 zimekamilika ubao unasoma Yanga 1-0 Geita Gold na ni kipindi cha pili wameokota nyavuni bao hilo.

Ni Fiston Mayele dakika ya 57 Uwanja wa Azam Complex limeivusha Yanga mpaka hatua ya nusu fainali itamenyana na Singida Big Stars.

Ushindi huo unawafanya Yanga kuwavuruga Geita Gold nje ndani kwenye mechi ambazo wamekutana ilikuwa ile ya ligi mizunguko yote miwili walishinda na leo mchezo wa tatu ni wa robo fainali.