SIMBA inatinga hatua ya nusu fainali Azam Sports Federation kwa ushindi wa 5-1 Ihefu.
Ni mchezo ambao umechezwa Uwanja wa Azam Complex huku ukishuhudia matumizi makubwa ya nguvu kwa wachezaji wa pande zote mbili.
Mabao ya Simba yamepachikwa na Jean Baleke ambaye ametupia mabao matatu kwenye mchezo wa leo.
Saido Ntibanzokiza katupia bao moja kipindi cha kwanza.
Ngoma ilianza na Baleke dakika ya 2,15 na 27 huku lile la Saido ikiwa ni dakika ya 40.
Ihefu walikuja kivingine kipindi cha pili na kupata bao kupitia kwa Roth dakika ya 61 akiunganisha krosi iliyopigwa na Nivere Tigere.
Bao la tano kwa Simba limefungwa na Pape Sakho aliyekamilisha ushindi huo dakika ya 90.
Sasa Simba itakutana na Azam FC kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali Azam Sports Federation