SIMBA MIKONONI MWA MABINGWA CAF

WAKIWA na hesabu za kuvaana na Ihefu kesho mchezo wa Khatua ya robo fainali Azam Sports Fedration wameshatambua kigongo watakachokutana nacho kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ni Wydad Athletic Club hawa watamenyana na Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira kwenye mchezo wa hatua ya robo fainali.

Baada ya droo kuchezwa nchini Misri tayari Simba imetambua kwamba ina kibarua kizito cha kusaka ushindi dhidi ya mabingwa watetezi.

Timu hiyo kete yake ya mwisho hatua ya makundi ilinyooshwa na Raja Casablanca 3-1 mchezo uliochezwa Uwanja wa Mohamed V.

Simba itaanzia nyumbani mchezo wa kwanza kati ya Aprili 21-22 huku mchezo wa pili ukitarajiwa kuchezwa kati ya Aprili 28-29 ugenini.