UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa yaliyotoea Morocco yote ni somo kwao na sasa macho yao ni kwenye mchezo wao dhidi ya Ihefu ambao ni wa robo fainali Azam Sports Federation.
Simba imetoka kufunga kete ya sita hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Mohamed V ukisoma Raja Casablanca 3-1 Simba lakini imetinga hatua ya robo fainali.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kilichotokea kwenye mchezo huo kimeshapita na sasa akili zao ni kwenye mchezo wao dhidi ya Ihefu.
“Habari za matokeo ugenini hizo zimeshapita akili zetu na macho yetu ni kwenye mchezo wetu dhidi ya Ihefu ambao ni wa Kombe la Azam Sports Federation tutafanya kazi kutafuta ushindi.
“Wachezaji wamepata uchovu kutokana na safari yetu ya Morocco kuwa ni ya kupanda na kushuka hivyo watapata muda wa kupumzika kisha watarejea kambini kuanza na maandalizi ya mchezo dhidi ya Ihefu,” .
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 7 Uwanja wa Uhuru kisha watakutana nao kwa mara nyingine Aprili 10 mchezo wa ligi.