Home Sports CHAMPIONSHIP NI YETU SOTE INATUHUSU

CHAMPIONSHIP NI YETU SOTE INATUHUSU

USHINDANI uliopo ndani ya Championship ikiwa ni mzunguko wa 25 unazidi kuleta raha ya kuifuatilia na kuona namna gani kila mmoja anavuna kile alichopanda.

Kila timu inapambana kwa nafasi yake kutafuta ushindi kwa kuwa hakuna timu inayopenda kubaki pale ambapo ipo kwa muda mrefu ukizingatia kwamba kupanda daraja ni mafanikio.

Uendeshaji wake ulivyo na namna ambavyo kila timu zinapambania malengo ndani ya Championship inaleta burudani kwelikweli.

Kikubwa kwa timu ambazo bado zipo nafasi ya chini kwa sasa ni lazima benchi la ufundi kutafuta mbinu mpya itakayowapa matokeo mazuri ndani ya mechi ambazo watacheza kwa sasa. Pia na wadau kutoa sapoti kwani hizi ni timu ambazo zinatuhusu pia.

Huku Championship kuna wachezaji wazuri ambao wakipewa nafasi watakuwa ni faida kwa taifa hasa kwenye timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo inawajumuisha Watanzania wote.

Tukumbuke kwamba kupanda kwenye ligi ni ndoto za timu nyingi shiriki ambazo zipo kwa sasa ila mbinu zinahitajika kwa kila timu kufanikisha hayo.

Muhimu kuona kwamba kila timu inapambana kwa vitendo kufikia ndoto hizo na sio kuishia kupiga porojo ilihali mambo bado hayajawa sawa kwenye mipango.

Hakuna timu ambayo haina nafasi ya kupanda mpaka Ligi Kuu Bara kila timu ina nafasi. Ili iweze kupanda mpaka kushiriki ligi kuu kwa msimu ujao ni lazima ifuate kanuni ambazo zipo kwenye kila safari ya mafanikio.

Juhudi isiyo kuwa ya kawaida katika kusaka matokeo pamoja na nidhamu ndani ya uwanja. Muhimu ni kwamba hakuna ambaye anaweza kufikia malengo ikiwa hatakuwa na nidhamu katika kuyatimiza itakuwa nii ngumu.

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limekuwa likifanya kazi kwa kuanzia kwenye Ligi Kuu Bara mpaka Championship hivyo hili linaleta picha kwamba mafanikio yanakuja pia.

Endapo jicho kubwa litakuwa ndani ya ligi pekee na kuacha huku kwenye kiwanda cha kutengeneza timu shiriki bila kujali maisha yao itakuwa ni hatari kwa afya ya soka letu.

Ili soka liendelee ni lazima kuwe na misingi makini ambayo inaanzia huku chini na haijengwi kwa kubahatisha bali mipango makini na hesabu zenye uhakika.

Timu shiriki ndani ya Championship ni lazima zitambue namna gani zinaweza kufikia malengo yao hasa ukizingatia kwamba siku zinakwenda kasi na hazisubiri kwa yale makosa ambayo yamepita ni lazima yafanyiwe kazi.

Zile ambazo zinaamini kwamba zina nafasi ya kupenya na hazina mtu wa kuzitazama zina jukumu la kutazama mbinu pekee ya ushindi kwenye mechi zao.

Njia ya kupata ushindi kwao ni moja tu kupambana na kufanyia kazi makosa yao ambayo waliyafanya kwenye mechi zao za mwanzo ikiwa walipata matokeo wana kazi ya kuendeleza rekodi ya kucheza bila kupoteza..

Nidhamu kwa wachezaji kwenye mechi zao zote bila kujali wanacheza na nani ni mbinu za kuwafanya wawe makini na bora kwenye matokeo ambayo wanayapata kwenye ligi.

Endapo hakutakuwa na nidhamu kwa wachezaji itasababisha wengi washindwe kufikia malengo kwani mchezo wa mpira ni kitu ambacho kinawategemea wachezaji na mashabiki nao wana mchango wao pia.

Mashabiki ni muhimu kuwa na timu hizi bega kwa bega na kuzishangilia bila kukata tamaa kwa kuwa matokeo mazuri yapo na mabaya pia yanahusika licha ya kwamba hakuna anayependa kuona inakuwa namna hiyo.

Kikubwa ni wachezaji kujituma na kufanya kazi kwa juhudi ili kufanikisha malengo ya timu kupanda ama kubaki hapo kwa ajili ya kuongeza nguvu kwa wakati ujao.

ReplyForward

Previous articleVIDEO:MSIKIE MZEE MUCHACHU KUHUSU USAJILI
Next articleUkicheza Kasino ya Mtandaoni Meridianbet unapata Mgao wa Tsh 5m Bure