KIKOSI cha Simba kimewasili salama Dar baada ya kutoka nchini Morocco walipokuwa na mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba ilikuwa na kete ya mwisho ilikuwa dhidi ya Raja Casablanca ugenini na ilishuhudia ubao wa Mohamed V ukisoma Raja 3-1 Simba.
Bao la Simba lilipachikwa na Jean Baleke dakika ya 48 katika mchezo ambao nahodha aliyepewa kitambaa alikuwa ni Shomari Kapombe.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kwa sasa hesabu zao ni mchezo wao ujao dhidi ya Ihefu ambao ni wa Kombe la Azam Sports Federation hatua ya robo fainali.