>

FOUNTAIN GATE KUIBUKIA AFRIKA KUSINI

TIMU ya Wasichana ya Shule ya Fountain Gate chini ya umri wa miaka 15, inatarajiwa kuondoka nchini Aprili 2 kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya Mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa shule za Sekondari.

Timu hiyo inakwenda katika Mashindajo hayo baada ya kufanikiwa kuwa Mabingwa wa Ukanda wa CECAFA kwa shule za Sekondari kwenye mashindano yaliyofanyika mwezi Febuari mwaka huu katika Viwanja vya Azam Complex.

Kocha wa Timu hiyo ya Fountain Gate Veronica Kyondo ameeleza namna ambavyo amewandaa wachezaji wake huku akidhamiria kufanya vyema katika Mashindano hayo.

Kwa upande wake Kelvin Shaban Heri ambaye ni Mratibu wa timu ya Wasichana ya Fountain Gate ameeleza utaratibu mzima wa safari huku Mashindano yakitarajiwa kufanyika katika Mji wa Durban.

“Sisi ni mabingwa tunakwenda kuonyesha ushindani na tunahitaji matokeo mazuri hivyo Watanzania wazidi kutuombea maandalizi yapo vizuri,”.