UTARATIBU WA KUINGIA KWA MKAPA LEO HUU HAPA

CLIFORD Ndimbo, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) amesema utaratibu wa kuingia kwa mashabiki Uwanja wa Mkapa utaanza saa sita kamili.

Leo timu ya Taifa ya Tanzania ina kiarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo dhidi ya Uganda ambao ni wa kuwania kufuzu Afcon.

Kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Misri uba ulisoma Uganda 0-1 Tanzania na mtupiaji akiwa ni Simon Msuva leo unapigwa saa 2:00 mchezo huo.

Ni jambo la nchi ambapo wadau wamenunua tikete zote upande wa mzunguko hivyo ni suala la mashabiki kuingia uwanjani kushangilia mwanzo mwisho.

“Ni jambo la nchi na utaratibu upo wazi kuanzia saa sita mchana mageti yatakuwa wazi, mashabiki wa Stars watakuwa na chaguo la kuingia kwenye mageti yote yatakayokuwa wazi.

“Jukumu lao ni moja kwenda kwenye jukwaa la mzunguko kisha kuanza shangwe mpaka mwisho wa mchezo kuwapa nguvu wachezaji,”.