STARS YAPOTEZA KWA MKAPA

JITIHADA za timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars kusaka ushindi dhidi ya timu ya taifa ya Uganda zimegonga mwamba.

Kwenye mchezo wa leo Machi 28,2023 uliochezwa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ubao umesoma Tanzania 0-1 Uganda.

Mchezo wa leo Stars ilikuwa kwenye umaliki mzuri huku nafasi chache zikitengenezwa kutoka kwa viungo pamoja na washambuliaji.

Ni bao moja pekee la nyota wa Uganda Rogers katika dakika za lala salama zimetosha kuipora Stars pointi tatu nyumbani.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo uliopita Uganda ikiwa nyumbani ilipoteza kwa kufungwa bao moja mtupiaji akiwa ni Simon Msuva.