Kikosi cha Simba SC, kimeanza safari leo Machi 28 kuelekea nchini Morocco kuifuata Raja Casablanca kwenye mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa usiku wa kuamkia Aprili Mosi 2023 nchini Morocco.
Msafara ambao unaondoka leo kupitia Qatar una jumla ya wachezaji 13 ikiwa ni pamoja na Kibu Dennis, Moses Phiri,Kennedy Juma.
Juma Mgunda, kocha msaidizi wa Simba amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao utakuwa na ushindani mkubwa.
“Tunatambua mchezo utakuwa mgumu lakini maandalizi ambayo tumefanya yanatupa nguvu ya kupata matokeo vijana wapo tayari,”.