KOCHA YANGA OUT

UONGOZI wa Klabu ya Yanga umetangaza kufikia makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na kocha mkuu wa Yanga Princess, Sebastian Nkoma.

Kwa mujibu wa taarifa ya klabu hiyo, kwa sasa kikosi hicho kitakuwa chini ya kocha Fredy Mbuna mpaka mwisho wa msimu.

Kocha huyo aliibuka ndani ya kikosi hicho akitokea kuinoa Simba Queens ambao walitwaa ubingwa wa Ligi ya Wanawake.

Akiwa na timu hiyo amekutana mara mbili na Simba Queens huku akisepa na pointi mbili na mabao mawili ya kufunga.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza walitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1 na ule wa pili wa mzunguko wa pili ngoma ilikuwa ni 1-1.