NGOMA ni nzito kwa makocha wawili wa mitaa ya Kariakoo, Robeto Oliveira wa Simba na Nasreddine Nabi wa Yanga kwenye anga za kimataifa kutokana na kila mmoja kutusua na wachezaji wake kwenye anga la utupiaji.
Ni wale wa Simba wanaongoza kumsimamisha Rob ambapo ni mara 9 alinyanyuka kwenye benchi kufurahia mabao yaliyozamishwa kimiani.
Mwamba wa kwanza kumpa furaha alikuwa ni Henock Inonga ilikuwa dhidi ya Vipers ugenini dakika ya 9 kisha akafuata Clatous Chama ilikuwa Uwanja wa Mkapa dhidi ya Vipers.
Wengine ambao walipachika mabao kwenye mechi za kimataifa ni Chama tena alitupia mabao matatu kwenye mchezo dhidi ya Horoya, Sadio Kanoute na Jean Baleke hawa walitupia kambani mabao mawilimawili Uwanja wa Mkapa.
Yanga mastaa waliompa tabasamu Nabi wa kwanza alikuwa ni Kennedy Musonda mchezo dhidi ya TP Mazembe uliochezwa Uwanja wa Mkapa waliposhinda mabao 3-1 wengine ni Mudhathir Yahya na Tuisila Kisinda hawa walitupia mojamoja.
Dhidi ya Real Bamako Fiston Mayele alitupia mabao mawili ugenini na Jesus Moloko naye alimnyanyua Nabi dhidi ya US Monastir ni Mayele tena alitupia na Musonda.
Ni Rob amepata tabu kwa furaha kushangilia mabao waliyofunga ambayo ni 9 huku Nabi mastaa wake wakifunga mabao 8.
Kwenye upande wa ulinzi ngoma ni nzito kwa wote kwa kuwa ni mabao mannemanne Aishi Manula wa Simba na Diarra Djigui wa Yanga wametunguliwa.