>

UGANDA 0-0 STARS

UBAO wa Uwanja wa Suez Canal huko Ismailia Misri unasoma Uganda 0-0 Tanzania.

Ni mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2023 nchini Ivory Coast ambapo timu zotezinasaka pointi tatu.

Mchezo ambao upo wazi kwa timu zote kupata matokeo kutokana na nafasi ambazo zinatengenezwa.

Uganda wanaonekana kuwa imara hasa kwa kupeleka mashambulizi mara kwa mara mbele ya Stars huku wakiwa wamepata kona zaidi ya tatu.

Stars wanashambulia kwa kushtukiza huku wakimtumia Novatus Dismas kwenye mapigo huru.

Simon Msuva ni miongoni mwa staa wa Stars ambao wanapambana kwa kushirikiana na Mbwana Samatta kwenye eneo la ushambuliaji.