>

STARS YASEPA NA POINTI DHIDI YA UGANDA UGENINI

KAZI kubwa kwa vijana imefanywa kupambania nembo ya Tanzania na kufanikiwa kupata ushindi.

Ubao wa Uwanja wa Suez Canal huko Ismailia Misri baada ya dakika 90 umesoma Uganda 0-1 Tanzania.

Bao pek
Ni mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2023 nchini Ivory Coast ambapo timu zotezinasaka pointi tatu.

Mchezo ambao upo wazi kwa timu zote kupata matokeo kutokana na nafasi ambazo zinatengenezwa.

Uganda wanaonekana kuwa imara hasa kwa kupeleka mashambulizi mara kwa mara mbele ya Stars huku wakiwa wamepata kona zaidi ya tatu.

Bao pekee la ushindi limefungwa na Simon Msuva dakika ya 69 akitumia pasi ya Dickson Job aliyetoa pasi mpenyezo akiwa nje ya 18.

Stars yenye Mbwana Samatta ilicheza kwa kujilinda huku ukuta wao ukiongozwa na Bakari Mwamnyeto akishirikiana na Job pamoja na Ibrahim Bacca.

Kazi kubwa wamefanya mabeki wa Stars kuiweka ngome salama huku Aishi Manula akiwa imara kwenye kuokoa hatari za nyota wa Uganda waliokuwa wanaongozwa na Emmanuel Okwi.