BAADA ya kufanikiwa kufuzu hatua ya Robo Fainali ya Kombe la Shiriko Afrika, uongozi wa Yanga umeibuka na kutamka kuwa levo ambazo wanazo, wao sio wa kuihofia timu yoyote.
Kauli hiyo imekuja mara baada ya Yanga kuwafunga mabao 2-0 US Monastir ya Tunisia katika mchezo wa tano wa Kundi D kunako Kombe la Shirikisho Afrika uliochezwa juzi Jumapili, Uwanja wa Mkapa, Dar.
Yanga imefuzu hatua hiyo, ikiwa bado ina mchezo mmoja dhidi ya TP Mazembe baada ya kukusanya pointi 10 sawa na US Monastir.
Akizungumza na Spoti Xtra, Ofisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe, alisema: “Ninaamini baadhi ya timu zitakuwa zimejifunza jinsi ya kuzifunga timu za Waarabu baada ya sisi kuwafunga US Monastir mabao 2-0.
“Kwa levo ambazo tumezifikia Yanga, sisi hatuihofii timu yoyote bali sisi ndio tunahofiwa, hiyo inaonesha ni jinsi gani tuna kikosi bora msimu huu.
“Hivyo Wanayanga waondoe hofu, kwani tofauti na wachezaji bora tuliokuwa nao, pia tuna benchi bora kla ufundi linaoongozwa na Nabi (Nasreddine).”