AZAM FC NA MWENDO WAO ULEULE

MSIMU huu pia haujawa mzuri kwa Azam FC ambayo kila wakati huwa inaanza kwa kuleta ushindani mkubwa.

Mateso makubwa ambayo huwa wanapitia kwenye mechi za ugenini bado hawajapata majibu yake hivyo wana kazi ya kuboresha zaidi ili wakati ujao kuwa imara.

Miongoni mwa sababu ambazo zimekuwa zikiwapa ugumu Azam FC ni pamoja na kushindwa kutumia nafasi ambazo wanazipata na yale makosa ya waamuzi ambayo yanaitwa ya kibindamu.

Kwa mfano kwenye mchezo dhidi ya Tanzania Prisons waliopoteza ugenini ni moja ya mchezo amao ulisababisha Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit kufungiwa miezi mitatu kwa kile kilichoelezwa kuwalalamikia waamuzi.

Ukitazama mchezo dhidi ya Yanga ule wa mzunguko wa kwanza mpira ulikuwa unaonekana umetoka nje lakini mwendo uliendelea na mwisho wa siku Azam FC wakafungwa bao moja kwenye sare ya kufungana mabao 2-2.

Sio Yanga tu kuna msimu Simba ilisepa na pointi tatu za Azam FC kwa bao la Meddie Kagere aliyetumia krosi ya Shomari Kapombe ambayo ilionekana mpira ulikuwa nje ya mstari.

Yote kwa yote Azam FC ina kazi nyingine kujipanga kwa msimu wa 2023/24 kwa kuwa hakuna matumaini ya kutwaa ubingwa wa ligi kwa sasa.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya 4 pointi zake ni 47 baada ya kucheza mechi 25.