AL AHLY WAMEPIGWA HUKO LIGI YA MABINGWA AFRIKA

MAAJABU ya mpira kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika yameendelea ikiwa ni hatua ya makundi.

Ni Marcelo Allende alipachika bao la mapema dakika ya 4, ngoma nyingine ilijazwa kimiani na Themba Zwane dakika ya 24, Teboho Mokoena alipachika dakika ya 40 kwenye mchezo dhidi ya Al Ahly.

Ni Peter Shalulile alijaza kimiani mara mbili dakika ya 72 na 88 huku yale ya Al Ahly yakifungwa na Mohamed Sharif dakika ya 13 na Percy Tau dakika ya 61.

Ubao wa Uwanja wa Loftus Versfeld umesoma Mamelod Sundowns 5-2 Al Ahly katika kundi B.

Jumla Sundown wanafikisha pointi 10 nafasi ya kwanza huku Al Ahly wakiwa na pointi 4 nafasi ya tatu ile ya pili ni mali ya Al Hilal yenye pointi 9.