KIKOSI cha Simba leo Machi 9 2023 kimeibukia Morogoro kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar.
Chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira mapema leo kilifanya mazoezi kabla ya kuanza msafara wa kuelekea Moro mji kasoro bahari.
Huu ni mchezo wa mzunguko wa pili ambao unatarajiwa kuchezwa Jumamosi saa 10:00 jioni Uwanja wa Manungu.
Kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa Simba ilisepa na pointi tatu mazima hivyo ina kibarua pale Manungu.
Msimu uliopita waligawana pointi mojamoja kwa ubao kusoma Mtibwa Sugar 0-0 Simba zama za Pablo Franco.