KMC WAICHAPA KAGERA SUGAR

HATIMAYE leo Machi 9,2023 KMC imepata ushindi mbele ya Kagera Sugar na kusepa na pointi tatu mazima.

KMC haikuwa kwenye mwendo mzuri kwenye mechi zake za hivi karibuni ambapo ilipotoka kunyooshwa bao 1-0 dhidi ya Yanga ikapoteza pia mbele ya Azam FC kwenye mechi za ligi ilizocheza Dar.

Ni mabao ya Daruesh Saliboko dakika ya 8 na 45 Uwanja wa Uhuru yametosha kuipa pointi tatu KMC inayonolewa na Hitimana Thiery.

Ushindi huo unawaondoa kwenye nafasi ya 13 ambayo walikuwa na pointi zao 23 sasa wanagotea nafasi ya 11 wakiwa na pointi 26.

Kazi bado ni nzito kwenye mechi zilizobaki kutokana na ushindani kuwa mkubwa na ligi kuwa kwenye lala salama.