YACOUBA ATWAA TUZO YA MCHEZAJI BORA

NYOTA Yacouba Songne amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Februari ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara.

Yacouba kwa sasa yupo ndani ya Ihefu ambapo aliibuka hapo akitokea kikosi cha Yanga ambapo alisitisha mkataba wake.

Ni Meddie Kagere wa Singida Big Stars na Elias Maguli wa Geita Gold hawa alikuwa nao kwenye fainali wakishindania tuzo hiyo.

Kwa mujibu wa Kamati ya Tuzo iliyo chini ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) imempitisha Yacouba kutwaa tuzo hiyo kwa mwezi Februari.

Yacouba ameanza vizuri ambapo alifunga bao kwenye sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Singida Big Stars na waliposhinda mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji.