UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa mashabiki ni muhimu kwenye mchezo wao dhidi ya Vipers ambao ni Ligi ya Mabingwa Afrika.
Simba ina kibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Vipers unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba, Ahmed Ally amesema kuwa kila mtu atatimiza wajibu wake kupata ushindi na wapinzani wao Vipers hawatatoka salama.
“Kila mmoja atimize wajibu wake, makocha watatimiza wajibu wao, kina Bocco watatimiza wajibu wao na sisi kama mashabiki tutimize wajibu wetu. Tukiunganisha nguvu Vipers hawawezi kutoka salama kwenye ardhi ya Tanzania.
“Simba malengo yetu upata matokeo chanya na kusonga mbele Simba kufeli kwetu ni robo fainali, sio hatua ya makundi.”