AZAM FC KWENYE KAZI DHIDI YA MAPINDUZI

AZAM FC leo ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa 16 bora ASFC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

Itakuwa ni dhidi ya Mapinduzi saa 1:00 usiku ambapo mshindi atatinga hatua ya rob fainali.

Miongoni mwa wachezaji ambao wapo tayari kwa mchezo huo ni pamoja na Abdul Suleiman, ‘Sopu’, Prince Dube,Sospeter Bajana.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Azam FC, Kali Ongala amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo na wanahitaji ushindi.

“Wachezaji wapo tayari na wanatambua umuhimu wa kombe hivyo tutaingia kwa umakini kusaka ushindi kwenye mchezo wetu,”