MABEKI wawili kwa sasa ndani ya Ligi Kuu Bara wanaongoza kwa pasi ndefu za uhakika kwenye mechi za ligi.
Nyota hawa wamekuwa wakifanya hivyo kwenye mechi ambazo wanacheza jambo ambalo linaongeza nguvu kwa timu hizo kufanya mashambulizi kuanzia nyuma kwenda mbele.
Pia wamekuwa wakiweka uimara kwenye lango lao ndani ya dakika 90 kwenye kutimiza majukumu yao.
Ni Pascal Wawa nyota wa Singida Big Stars ambaye ni raia wa Ivory Coast.
Beki huyo kitasa amewahi kukipiga ndani ya kikosi cha Simba ambacho kwa sasa kinanolewa na Kocha Mkuu, Roberto Oliveira.
Pia yupo Kelvin Yondani huyu ni mali ya Geita Gold akiwa kwenye kazi ya kutimiza majukumu yake.
Timu zote mbili zimetinga hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho.