SIMBA KWENYE KIBARUA KINGINE UHURU

MACHI 2 2023 kikosi cha Simba kina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya African Sports.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Uhuru kwa kuwa Uwanja wa Mkapa unafanyiwa maboresha na utatumika kwa mechi za kimataifa.

Simba inaingia kwenye mchezo huo ikiwa inakumbuka kwamba ilitinga hatua hiyo kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union.

Moja ya mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa na kila timu ilicheza kwa umakini huku Simba ikipata nafasi ya kufunga bao hilo kupitia kwa Sadio Kanoute, kiungo mgumu ndani ya kikosi hicho.

Tayari kikosi cha Simba kimerejea Dar kikitokea Uganda kilipokuwa na kazi ya kusaka ushindi dhidi ya Vipers mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Robert Oliveira, Kocha Mkuu wa Simba ameweka wazi kuwa anahitaji ushindi kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Alhamisi.