KWA mara nyingine tena Salim Abdallah Muhene wengi wanapenda kumuita Try Again atasalia kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ndani ya Simba.
Februari 27, Rais wa heshima wa Simba Mohammed Dewji amemteua tena Salim Try Again kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba.
Mo amesema ana imani na Mwenyekiti Muhene kuwa ataiongoza Simba kufikia mafanikio makubwa zaidi Afrika na duniani.
Pia kwenye hafla hiyo wale viongozi ambao walikamilisha muda wao na uchaguzi kufanyika walipewa pongezi.
Miongoni mwao wataendelea kuwa ndani ya Bodi ya Wakurugenzi baada ya kuchaguliwa kwa mara nyingine tena.
Ni Murtanza Mangungu huyu amesalia kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Simba, Asha Baraka huyu amesalia kwenye nafasi ya mjumbe wa Bodi.
Simba kwa sasa kikosi chake kipo hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika mchezo wake uliopita kilipata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Vipers ugenini na kusepa na pointi tatu.
Kila la kheri Try Again na viongozi wengine