MECHI za nyumbani kwenye anga za kimataifa zina umuhimu mkubwa kwa wawakilishi kimataifa kupata ushindi kuzidi kujiongezea hali ya kupata nafasi kutoka kwenye hatua ambayo wapo.
Hatua ya makundi ni kituo kinachowasafirisha wawakilishi mpaka hatua ya robo fainali ambayo inaongeza thamani kwa wachezaji pamoja na timu kuzidi kuwa bora.
Ushindi kwenye mechi za nyumbani ni muhimu kwa kila mmoja kufanya kweli na inawezekana kwa wachezaji kutimiza majukumu yao.
Mechi za nyumbani kete muhimu kupangwa kupata ushindi ni jambo la msingi kwa kuwa wanaifanya kazi kwenye mechi zinazofuata kuzidi kuongeza hali ya kujiamini.
Simba walianza kwa kupata matokeo mabaya nyumbani wana kazi nyingine dhidi ya Vipers Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo huu zile porojo zinapaswa kutupwa kule.
Angalau Yanga kwenye Kombe la Shirikisho wao walipata ushindi dhidi ya TP Mazembe imewapa hali ya kujiamini na kwa mechi zijazo wana imani ya kuendelea pale walipoishia.
Ugenini kuhesabu unakwenda kupata ushindi kwenye mechi za kimataifa hasa kwa bara letu la Afrika ni nadra sana licha ya kila kitu kuwa wazi bado kuna michezo mingine ambayo inawatoa nje ya uwanja wachezaji.
Kila mtu anatamba kwao iwe hivyo kwa wawakilishi wetu pia wakiwa nyumbani wanapambana kushinda kwa nguvu kisha wakitoka wanakwenda kumalizia kazi ambayo walianza nyumbani.
Malengo ya kutinga robo fainali ni makubwa lakini hayatatimia ikiwa hakutakuwa na mipango makini hasa kwa mechi za nyumbani.