BAADA ya kukamilisha dakika 90 za kimataifa ugenini tayari kikosi cha Simba kimerejea Dar.
Februari 25,2023 kilishuka Uwanja wa St Mary’s kusaka pointi tatu dhidi ya Vipers ukiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi.
Baada ya dakika 90 ubao ulisoma Vipers 0-1 Simba huku mtupiaji akiwa ni Henock Inonga aliyepachika bao hilo dakika ya 19.
Miongoni mwa nyota ambao wapo kwenye msafara huo ni Peter Banda ambaye alianza benchi kwenye mchezo huo.
Clatous Chama, Sadio Kanoute, Mzamiru Yassin hawa walianza kwenye kikosi cha kwanza.