Home International YANGA NDANI YA MALI KUWAVAA BAMAKO

YANGA NDANI YA MALI KUWAVAA BAMAKO

MSAFARA wa Yanga ndani ya Mali kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika unaotarajiwa kuchezwa Februari 26.

Kikosi hicho kilikwea pipa na Shirika la Ndege la Ethiopia tayari kwa ajili ya kuwavaa Real Bamako.

Yanga ina pointi tatu kibindoni baada ya kupata ushindi kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe na ilitunguliwa mchezo wa kwanza ugenini dhidi ya US Monastri ambapo ilichapwa mabao 2-0.

Baada ya kuwasili nchini Mali walifanya mazoezi ya kurejea kwenye utimamu wa mwili kwa ajili ya mchezo wao ujao ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Kwenye Kundi D Real Bamako wao wana pointi moja kibindoni walilazimisha sare dhidi ya US Monastri.

Miongoni mwa mastaa ambao wapo kwenye msafara ni pamoja na Kibwana Shomari, Djigui Diarra, Metacha Mnata.

Ally Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo wanatambua utakuwa na ushindani mkubwa.

“Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu ujao ambapo tunajua utakuwa na ushindani mkubwa, wachezaji wanajua ambacho tunahitaji ni ushindi.

“Mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi kwenye mchezo wetu tuna amini tutafanya vizuri,”.

Previous articleWAARABU WAIBEBA YANGA MALI, PHIRI AVALISHWA MABOMU AWALIPUE VIPERS
Next articleVIDEO:KMC :TUNAPITA KIPINDI CHA MPITO,HATUJAKATA TAMAA