HII HAPA RATIBA LIGI KUU BARA

BAADA ya Mzizima Dabi kukamilika Februari 21 na ubao wa Uwanja wa Mkapa kusoma Simba 1-1 Azam FC leo Ligi Kuu Bara inatarajia kuendelea.

Ni mchezo wa wakusanya mapato KMC v Yanga unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, ubao ulisoma Yanga 1-0 KMC.

Hivyo mchezo wa leo KMC wataingia kusaka pointi tatu kulipa kisasi huku Yanga wakiwa na hesabu za kulinda rekodi yao ya ushindi.

Mechi nyingine za hivi karibuni kwenye ligi itakuwa namna hii:-Februari 24 Ruvu Shooting v Kagera Sugar

Dodoma Jiji v Ihefu