KOCHA Mkuu wa Yanga Nasreddine Nabi, amesema kuwa watabadili mbinu kwenye mchezo dhidi ya TP Mazembe, huku akija kwa utofauti kulingana na mchezo husika.
Nabi amesema kuwa kila mchezo una mbinu zake tofauti kulingana na aina ya wapinzani wanaokwenda kukutana nao jambo linalowapa nguvu ya kuingia uwanjani kusaka ushindi.
Leo, Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa pili dhidi ya TP Mazembe ambao wametoka kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Real Bamako.
“Tunacheza na timu ngumu na inahitaji matokeo lakini nasi tumejipanga kupata ushindi licha ya kwamba tutakutana na ugumu kutoka kwa wapinzani.
“Mashabiki wajitokeze kwa wingi kwa ajili ya mchezo wetu uwepo wao utaongeza nguvu kwa wachezaji kupambana na kushinda kwani hilo ndio jambo ambalo tunahitaji,” amesema.
Miongoni mwa wachezaji amao wanatarajiwa kuanza kwenye mchezo wa leo ni pamoja mshambuliaji Fiston Mayele huku langoni ikiwa ni Diarra kwa upande wa safu ya ulinzi akiwa ni pamoja na Dickson Job.