KIMATAIFA:YANGA 2-0 TP MAZEMBE

DAKIKA 45 bora kwa Yanga kutokana na kucheza soka la kushambulia na utulivu mkubwa dhidi ya TP Mazembe.

Ni uhakika kusepa na milioni 10 ambazo ni zawadi kutoka kwa Mama ambaye aliahidi kutoa kila M 5 kwa bao moja kwenye anga za kimataifa.

Ubao wa Uwanja wa Mkapa unasoma Yanga 2-0 TP Mazembe ambao hawaamini wanachokiona.

Ni mabao ya Kenedy Musonda dakika ya 6 na lile la pili ni mali ya Mudathir Yahya dakika ya 10 ikiwa ni mchezo wa hatua ya makundi Kombe la Shirikisho.