Christian Atsu: Mwili wake wapatikana kwenye vifusi baada ya siku 11 tangu tetemeko Uturuki

Mwili wa mwanasoka wa Ghana Christian Atsu umepatikana chini ya jengo alilokuwa akiishi kusini mwa Uturuki baada ya tetemeko kubwa la ardhi wiki iliyopita, wakala wa winga huyo wa zamani wa Chelsea alisema na kunukuliwa na Reuters.

“Mwili wa Atsu ulipatikana chini ya vifusi,” Murat Uzunmehmet aliwaambia waandishi wa habari huko Hatay, ambapo mwili wa mwanasoka huyo ulipatikana.

“Kwa sasa, vitu zaidi bado vinatolewa. Simu yake pia ilipatikana.” Atsu alikuwa amepanga kusafiri Kusini mwa Uturuki saa chache kabla ya tetemeko hilo kutokea, lakini alisema Ijumaa Mghana huyo aliamua kusalia na klabu hiyo baada ya kufunga bao la ushindi katika mechi ya Februari 5 ya ligi ya Uturuki (Super Lig).

Atsu aliwahi kuichezea Newcastle United pia.