KUELEKEA kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya Makundi kesho Februari 19,2023 uongozi wa Yanga umewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi.
Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo huo wa kimataifa wa pili wakiwa wametoka kupata maumivu kwenye mchezo wa kwanza ugenini.
Ni US Monastir 2-0 Yanga ilikuwa matokeo kwenye mchezo huo uliochezwa ugenini hivyo huu unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Yanga kucheza wakiwa nyumbani, Uwanja wa Mkapa.
Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Yanga, Ally Kamwe amesema:-“Mnajua kwamba mkizungumzia mabao mnamzungumzia Fiston Mayele, Wananchi jitokezeni kwa wingi Jumapili kuona burudani na kuwa nguvu wachezaji.
“Wachezaji wote wapo tayari na tutakuwa nyumbani tunaamini itakuwa kazi kubwa na nzuri kwa mashabiki kujitokeza kwa wingi kushuhudia kazi itakayofanywa na wachezaji,”