HAKUNA MWENYE KAZI NYEPESI KIMATAIFA

HAKUNA mwenye unafuu kwa sasa sio Simba wala Yanga kwenye anga za kimataifa kutokana na mechi zao wote kuwa ngumu.

Kwa mashabiki wakati huu lazima kuungana na kufanya kazi moja kushangalia timu zao huku wachezaji nao akili zao zikiwa kwenye mechi uwanjani.

Dakika 90 ni za jasho kubwa kutokana na umuhimu wa pointi tatu kwa kila timu ambayo inashuka kusaka ushindi na hakuna ambaye anapaswa kudhani ana kazi ndogo.

Kuna wachezaji ambao wanadhani wanakazi nyepesi tofauti na mpinzani kwenye mchezo huo kutokana na aina ya timu ambayo wanakutana nayo.

Hakika hakuna mwenye kazi ndogo, wote wana kazi kubwa na ngumu ndani ya dakika 90 hivyo lazima wajitoe kwa hali na mali kusaka ushindi.

Ushindi nyumbani ni zawadi kwa mashabiki na wapenda mpira kwa kuwa hakuna ambaye anatakuwa na furaha akiona timu yake imefungwa ikiwa nyumbani.

Kasumba ya kuamini kwamba kila mtu ashinde mechi zake bila vitendo hiyo ni mbaya na itawafanya wengi kuondoka uwanjani wakiwa na maumivu matokeo yakiwa tofauti.

Mechi zote ni ngumu sio kwa Simba wala Yanga muhimu kufanya kazi kweli na kutimiza yale maelekezo ambayo yatatolewa na benchi la ufundi.

Kazi ni ngumu kimataifa lazima kila timu ipambane kupata ushindi kwenye mechi zao kimataifa na inawezekana.

Kila la kheri wawakilishi wetu kwenye anga la kimataifa.

ReplyForward