KIKOMBE wanachokutana nacho wawakilishi wa Tanzania kwenye mashindano ya kimataifa ni cha moto ni muhimu kukishika kwa tahadhari na sio porojo.
Kwa Yanga ambao Jumapili watacheza dhidi ya TP Mazembe na Simba ambao watacheza dhidi ya Raja Casablanca wote wapo kwenye eneo gumu na wasipofanya maandalizi mazuri itakuwa ngumu kwao kupenya.
Nafasi za kushinda ni ndogo kutokana na kushindwa kutumia nafasi ambazo wamekuwa wakizitengeneza pamoja na wapinzani wao kutokuwa na presha kutokana na mtaji wa pointi walizonazo.
Jambo ambalo linapaswa kufanyika kwa wawakilishi wa Tanzania kwenye anga la kimataifa ni kutulia na kutumia nafasi zile watakazopata kwa umakini.
Huku katika anga la kimataifa ukipoteza mchezo mmoja unapoteza na hali ya kujiamini kutokana na kila muda kucheza kwa presha.
Ukubwa wa timu ambazo zitakuja Uwanja wa Mkapa uwapo hasira wawakilishi wa Tanzania kucheza kwa umakini na kuchukua pointi tatu.
Kwenye porojo ni rahisi sana kuchukua pointi tatu lakini kwenye matendo hapo ugumu upo kwa kuwa hata wapinzani wenyewe wanazitaka pointi tatu.
Jambo linalotakiwa ni kila mmoja kucheza karata yake kwa hesabu kubwa kuelekea mechi hizo za kimataifa ambazo zinasubirwa kwa shauku kubwa.
Furaha ya mashabiki ipo kwenye ushindi na furaha ya wachezaji ipo kwenye kushinda basi muda huu ikawe kwa vitendo na kila mmoja afanye kazi yake kwa umakini.