MAJEMBE HAYA YA KAZI KAMILI SIMBA KUIVAA HOROYA

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kilakitu kinakwenda sawa na wachezaji wote wapo tayari.

“Wachezaji wetu ambao tuliwakosa kwenye mchezo uliopita dhidi ya Horoya ugenini ikiwa ni pamoja na Saido Ntibanzokiza wapo tayari ambapo Saido ameanza mazoezi.

“Peter Banda anasubiri ripoti ya madaktari baada ya vipimo wao wataamua kama anaweza kuungana na wenzake ama la,” amesema.

Pia kiungo mkabaji Jonas Mkude naye pia ameanza mazoezi na kikosi hicho ambapo hakuwa sehemu ya msafara uliokuwa nchini Guinea.

Mkude ni miongoni mwa wakongwe ndani ya kikosi cha Simba huenda akapewa nafasi ya kuanza mchezo ujao ikiwa benchi la ufundi litaamua iwe hivyo.