>

YANGA KUTUA DAR

MSAFARA wa kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi leo Februari 14 unatarajiwa kuwasili Dar.

Wawakilishi hao wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho Afrika walikuwa nchini Tunisia kwa ajili ya dakika 90 dhidi ya US Monastir.

Ubao ulisoma US Monastir 2-0 Yanga hivyo wanarejea wakiwa na hasira kuelekea kwenye mchezo ujao dhidi ya TP Mazembe ambao wapo nao kwenye kundi D.

Nyingine ni Real Bamako ambayo nayo ilipoteza kwenye mchezo wake wa kwanza dhidi ya TP Mazembe.

Februari 19,Uwanja wa Mkapa Yanga itakuwa na kibarua cha pili kwenye anga la kimataifa.

Miongoni mwa nyota ambao wapo kwenye msafara wa Yanga ambao ulipitia Dubai ni pamoja na Djuma Shaban, Khalid Aucho, Jesus Moloko, Kibwana Shomari na Dickson Job.