WAZEE WA MPAPASO KUENDELEZA VIPIGO

WAZEE wa mpapaso, Ruvu Shooting wametamba kuwa kwa sasa ni mwendo wa vipigo kwa kila watakayekutana naye.

Timu hiyo mchezo wake uliopita ikiwa Uwanja wa Jamhuri Morogoro ilishinda mabao 2-1 dhidi ya KMC.

Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire amesema kuwa hakuna atakayeweza kuwazuia kwa sasa kwenye mwendelezo huo baada ya kuwa kwenye mwendo usioridhishwa.

“Sasa tumerudi rasmi kwenye kazi wazee wa mpapaso, ushindi wetu dhidi ya KMC utatufanya tuendelee kutembeza vipigo kwa kila ajaye na inawezekana kwani tuna wachezaji wazuri.

“Hii ni Ruvu Shooting waambieni wapinzani wetu tunaendeleza vipigo ajaye ajiaandae kwa namna yoyote lazima akutane na mpapaso,” amesema.

Mchezo ujao kwa Ruvu Shooting unatarajiwa kuwa dhidi ya Geita Gold Uwanja wa Nyakumbu, Februari 17.