UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa unawatambua kwa umakini wapinzani wao Horoya kutokana na kuwasoma kwa muda kwenye mechi zao pamoja na mbinu ambazo wanacheza.
Simba leo Februari 11 ina kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa hatua ya makundi ikiwa kundi C na timu nyingine ni Vipers ya Uganda na Raja Casablanca ya Morocco.
Ahmed Ally Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba alisema kuwa kwenye anga la kimataifa wanahitaji kupata ushindi huku wakiwa na hesabu za kuanza vizuri.
“Wapinzani wetu Horoya tunawatambua kwa umakini ubora wao ulipo pamoja na uwezo wao nje ndani hivyo tunaamini benchi la ufundi litawapa mbinu za ushindi wachezaji wetu kwenye mchezo muhimu.
“Hakuna ambaye hapendi kuona tunapata matokeo mazuri kwa kuwa tunaanza ugenini tukitoka huko tunakuja kufanya kazi kwenye mechi ambayo tutacheza nyumbani mashabiki wazidi kutuombea,” amesema Ally.