JANA usiku vyombo mbalimbali ya Habari kutoka Uturuki vilitoa taarifa kuwa nyota wa kimataifa wa Ghana Atsu hakuwa ameokolewa kama ambavyo iliripotiwa awali.
Taarifa hizo zilikuja mara baada ya viongozi wa klabu yake ya sasa kuzunguka kwenye hospitali zote wakijaribu kumsaka bila mafanikio.
Inadaiwa Christian Atsu bado amekwama kwenye kifusi yeye na meneja wake na jitihada za uokoaji zikiwa bado zinaendelea kwake na watu wengine.
Atsu ni miongoni mwa waliopata na matatizo ya tetemeko kubwa la ardhi yaliyotokea Ututuki na Syriana kusababisha vifo vya watu zaidi ya 2000 na familia nyingi kukosa makazi.
Atsu ambaye ni nyota wa zamani wa Chelsea na Newcastle za England anakipiga kwenye Klabu ya Hatayspor inayoshiriki Ligi Kuu ya Uturuki.
Mungu awalinde ndugu zetu na wale ambao wapo kwenye majanga haya tuzidi kuwaombea kheri.